Related News
https://www.instagram.com/p/DReI4qOjH2-/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Stability returns to Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valdés Mesa amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 23 - 25 Januari, 2024.
Mara baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Mesa alipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb.)
Akiwa nchini, Mhe. Mesa atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete na pia atatembelea taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Mhe. Mesa pia atamtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere pamoja na kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa za viuadudu ya Biolarvicide cha Kibaha, Pwani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe. Mahendra Siregar jijini Jakarta, kwa ajili ya kuangalia hatua za mwisho za maandalizi ya Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itakayofanyika kuanzia tarehe 24-26 Januari, 2024 nchini humo.
Viongozi hao wamekubaliana kuwa maandalizi yote kwa ajili ya ziara hiyo yamekamilika na wako tayari kumpokea Mhe Rais tarehe 24 Januati atakapowasilo nchini Indonesia.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Waziri Makamba amesema ziara hiyo ni muendelezo wa Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kayika kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Indonesia ambao mwaka huu unatimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.
Ameongeza kuwa ziara hiyo pia inalenga kuimarisha Ushirikiano kati ya Tanzania na Indonesia katika maeneo ya kımkakati ya biashara, uwekezaji, Afya, elimu, uchumi wa buluu na kilimo.
Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe. Siregar amesema Indonesia iko tayari kumpokea Mhe Rais Samia nchini mwao na kuahidi kuwa Indonesia inauthamini uhusiano wake na Tanzania na itaendela kushirikiana kwa manufaa ya pande zote mbili.
Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa na ziara ya Kitaifa nchini Indonesia kuanzia tarehe 24-26 Januari 2024
TANZANIA, OMAN KUIMARISHA UTAMADUNI NA KUMBUKUMBU
Tanzania na Oman zimekubaliana kuimarisha sekta ya utalii kupitia utamaduni na kumbukumbu za mambo ya kale ili kuongeza utalii na kukuza uchumi wa mataifa hayo mawili kwa maslahi ya pande zote mbili.
Makubaliano hayo yameafikiwa na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Urithi wa Mambo ya Kale na Utalii wa Oman, Mhe. Salim Mohammed Al Mahrouq kujadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Oman katika ukumbi wa Wizara hiyo.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadiliana na kukubaliana kuongeza fursa na ushirikiano katika nyanja za mafunzo na uzoefu kwa wataalam wa pande zote mbili. Adha, katika Utekelezaji wa mambo hayo, viongozi na wataalam wa Tanzania na Oman watakutana hivi karibuni kupanga mikakati ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano.
Mazungumzo hayo ni hatua ya utekelezaji wa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab ya kukuza ushirikiano wa kidiplomasia na Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.
Mhe. Caesar Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amemtembelea Mhe. Jenelly Matundu (Mb), Naibu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Namibia kwa lengo na kujitambulisha na kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na Namibia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
@SuluhuSamia
akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Dkt. Abiy Ahmed uliowasilishwa kwake na Waziri na Mshauri – Sera wa Ethiopia Mhe. Taye Atske-Selassie Made mara baada ya kuwasili Ikulu, Dar es Salaam 6.11.2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Kibinadamu na Naibu Mratibu wa Huduma za Dharura Bi. Joyce Msuya, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 6 Novemba, 2023.

