Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi, Jenifa Omolo, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Maafisa Usafirishaji wa Wizara hiyo waliostaafu kazi hivi karibuni, ambapo aliwashukuru watumishi hao kwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili muda wote walipokuwa kazini. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Royal Village, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (kulia), kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi, Jenifa Omolo, akimkabidhi zawadi ya pongezi kwa Afisa Usafirishaji Mstaafu wa Wizara hiyo, Bw. Issa Abdallah (kushoto), kwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili muda wote alipokuwa kazini, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Maafisa hao waliostaafu kazi hivi karibuni. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Royal Village, jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha (kulia), wakitoa neno la shukrani na pongezi kwa Maafisa Usafirishaji wa wizara hiyo walistaafu hivi karibuni, ambapo waliwashukuru watumishi hao kwa kuwapa ushirikiano, kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili muda wote walipokuwa kazini. Hafla hiyo fupi ya kuwaaga watumishi hao imefanyika katika Hoteli ya Royal Village, jijini Dodoma.