SERIKALI KUKABILIANA NA UPANDAJI WA BEI ZA VYAKULA ZANZIBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imeanza kuchukua hatua kukabiliana na upandaji wa bei za vyakula hasa mchele na sukari nchini.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara wanaogiza vyakula nje ya nchi na watendaji wa Serikalini.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema matarajio ya Serikali ni kurudisha bei za awali kwa bidhaa zilizopo madukani, pia ameagiza Serikali kutoa fedha zake za kigeni na kuwapa kipaumbele wafanyabiashara hususan waagizaji vyakula nje ya nchi, hivyo amewataka wafanyabiashara hao kushirikiana kuagiza bidhaa hizo kwa pamoja.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi amegusia suala la mizigo kushukia bandari ya Mkoani ili kupunguza gharama za bidhaa Pemba .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *