WAZIRI DKT. NDUMBARO ATETA NA KATIBU MKUU WA CAF

Na Eleuteri Mangi, Cairo Misri

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya ziara katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Cairo nchini Misri.

Dkt. Ndumbaro amefanya ziara hiyo Septemba 25, 2023 ambapo amekutana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Ndg. Veron Mosengo-Omba na wamejadili masuala mbalimbali ya kuboresha mchezo wa soka nchini.

Waziri Dkt. Ndumabaro katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bi. Neema Msitha, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia pamoja na watumishi kutoka wizara hiyo na TFF.

    Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *