DKT. NDUMBARO ATETA NA WAZIRI WA MICHEZO MISRI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Vijana na Michezo wa nchini Misri Mhe. Ashraf Sobh Septemba 25, 2023 Jijini Cairo.

Viongozi hao wamekubaliana kushirikiana baina ya nchi hizo mbili hususan kubadilishana uzoefu na kutoa mafunzo katika Sekta ya michezo.

Aidha, Waziri na ujumbe wa Tanzania walipata wasaa wa kutembelea Kituo cha michezo cha Algazira Club ambacho kina viwanja mbalimbali vya kulea vipaji vya michezo kuanzia watoto wadogo hadi vijana ambao ni hazina kubwa ya wanamichezo katika taifa.

Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Ndumbaro aliambatana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT) Bi Neema Msitha, Mwenyekiti wa Baraza hilo Ndg. Leodigar Tenga, baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania pamoja na watumishi wa Wizara hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *