Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro amewakaribisha wananchi wa Jamhuri ya Watu wa China kujifunza Utamaduni na Lugha ya Kiswahili ambayo kwa sasa ni miongoni mwa lugha kubwa Duniani.
Mhe. Dkt. Ndumbaro ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza katika Tamasha la Utamaduni wa watu wa Jamhuri ya China lililofanyika Septemba 29, 2023 jijini Dar es Salaam.
Ameendelea kuwashukuru wananchi na Serikali ya Watu wa China kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika Sekta ya Utamaduni na Michezo ikiwemo ujenzi wa miondombinu ya michezo.