YANGA YATINGA HATUA YA MAKUNDI MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA

Na Eleuteri Mangi, WUSM , Dar es Salaam.

Timu ya Yanga imefuzu na kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuifunga timu ya El Merreikh ya Sudan kwa goli 1-0.

Mgeni Rasmi wa mchezo huo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amewaongoza Watanzania na mashabiki wa timu ya Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Septemba 30, 2023 katika uwanja wa Azam jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada kumalizika kwa mchezo huo Mhe. Mwinjuma amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekua mstari wa mbele katika kuimarisha shughuli za Michezo hapa nchini akibainisha kuwa Watanzania wana mwamko mkubwa na wanapenda Michezo.

Timu ya Yanga imetinga hatua hiyo ya makundi baada ya kujikusanyia alama Sita ambapo mchezo wa awali timu ya Yanga ilishinda goli 2-0 katika mchezo uliochezwa nchini Rwanda.

Mchezo huo umeshuhudiwa na Katibu Mkuu wa.Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *