Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni 500 ya Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) Ndg. Wallace Karia (kulia) ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa kwa Timu hiyo, baada ya kufuzu kucheza Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2023 yatakayofanyika nchini Ivory Coast mapema mwaka 2024. Katikati ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.