WAZIRI NDUMBARO AISISITIZA BASATA IENDELEE KUSIMAMIA MAADILI NA KUONGEZA MAPATO

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa ( BASATA) Prof. Saudin Mwakaje Oktoba 6, 2023 Jijini Dar es Salaaam.

Mhe. Ndumbaro amempongeza Prof Mwakaje kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza Baraza hilo, akimtaka ahakikishe Baraza linaendelea kuwa mshauri na mlezi katika Sekta ya Sanaa na kutekeleza majukumu yake mengine kwa manufaa ya wadau wa Sekta hiyo.

Kwa upande wake Prof Mwakaje amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi aliyompatia ya kuongoza Baraza hilo kwa nafasi ya Mwenyekiti na kuahidi kusimamia Baraza hilo kutekeleza majukumu yake ipasavyo, kwa kuwasaidia wasanii kunufaika na kazi zao pamoja na kuongeza mapato kwa Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *