MHE. NDUMBARO: WEKENI HISTORIA YA UKOMBOZI KATIKA RAMANI INAYOSTAHILI

Na Brown Jonas

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekielekeza Kituo Cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kuongeza ubunifu katika kuonesha mchango uliotolewa na Tanzania katika ukombozi wa nchi mbalimbali za Afrika.

Mhe. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo Oktoba 10, 2023 alipotembelea kituo hicho kuona namna kinavyotekeleza majukumu yake hususani kuhifadhi historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.

“Kituo hiki ni muhimu sana kwa nchi yetu kuonesha mchango wake katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika hivyo wekeni historia hii katika ramani inayostahili ili kuweka bayana mchango wa nchi yetu katika ukombozi wa Bara la Afrikaā€¯

Mhe. Ndumbaro amewataka watumishi wa kituo hicho kubadilisha namna ya utendaji kazi huku akiwasisitiza kuorodhesha vituo vyote 260 vilivyopo nchini ambavyo vilitumiwa na wapigania uhuru na kuvitangaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *