TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA FEDHA NA MAGAVANA WA BENKI KUU WA IMF

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayofanyika Marrakech nchini Morocco,

kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameshiriki mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF),

uliohudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Bi. Kristalina Georgieva, ambapo wamejadiliana fursa na changamoto zinazozikabili nchi zao na kupendekeza IMF iongeze ufadhili wa misaada na mikopo kwa nchi hizo ili ziweze kukabiliana na athari za majanga ya dunia na kutekeleza mipango yao ya kuharakisha maendeleo ya nchi zao na kupiga vita umasikini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *