WATANZANIA WANGA’RA NAGAI MARATHON 2023

Tanzania imeendelea kung’ara katika Mbio za Nagai Marathon 2023 zilizofanyika nchini Japan kufuatia Wanariadha wake kufanya vizuri katika mbio hizo zilizofanyika nchini humo leo Oktoba 15, 2023.

Katika Mbio za KM 42 (Full Marathon) Mwanariadha Peter Sulle ameibuka Kidedea na kufuatiwa na Mwanariadha Fabian Joseph.

Kwa upande wa Wanawake Mwanariadha Sara Ramadhan ameibuka mshindi.

Katika Mbio za KM 21 upande wa Wanaume Mwanariadha Josephat Gisemo ameibuka Kidedea ambapo nafasi ya pili imeenda kwa Damian Makiya, ambapo upande wa Wanawake Mwanadada Transfora Musa ameibuka mshindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *