NAIBU WAZIRI WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MHE. HAMIS MWINJUMA (MB) ATOA MAELEKEZO KWA OFISI YA HAKIMILIKI TANZANIA (COSOTA)

NAIBU Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (Mb) atoa maelekezo kwa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuhakikisha inapata mpango kazi wa utekelezaji wa majukumu kutoka kwa Kampuni ya Kukusanya Mirabaha ya kazi za Muziki iliyopewa Leseni ijulikanayo kama Tanzania Music Rights Society (TAMRISO) na kuhakikisha kuwa Kampuni hiyo nitatekeleza yote waliyoagizwa na Serikali. Aidha, alisisitiza kuwa vema kuhakikisha kuwa imewasilisha pia mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi ya kazi za Muziki ili kuwezesha ugawaji wa mirabaha.

Mheshimiwa Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo leo Oktoba 17, 2023 katika kikao chake na Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki, Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bi.Doreen Anthony Sinare alipotembelea Ofisini kupata taarifa ya masuala mbalimbali ya utendaji wa COSOTA.

Wakati akizungumzia suala la TAMRISO, Mh. Naibu Waziri alisema,

” Suala la TAMRISO kuwa na mfumo ni jambo la muhimu sana sababu mfumo ndiyo unasidia kujua nani anapata kiasi gani kulingana na matumizi ya kazi yake na Wasanii wengi wemekuwa wanalalamika hili hivyo ni lazima walete taarifa ya mfumo huo,” alisema Naibu Waziri Mhe. Mwinjuma.

Pamoja na hayo Mhe. Naibu Waziri Mwinjuma ameipongeza COSOTA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kukamilisha mchakato wa kuwezesha makusanyo ya Tozo ya Hakimiliki ( Copyright Levy) kuanza kufanyika toka tarehe 1.9.2023. Pia ameeleza kuwa Wizara itaendele na taratibu za kuomba Bunge kuridhia kuongezwa kea baadhi ya vifaa ambavyo havijaingizwa kwenye orodha ya awali vyenye matumizi makubwa katika kazi za sanaa ikiwemo Kompyuta, Simu, Flash, Harddrive, Vishikwambi na vinginevyo. Lengo likiwa ni Wasanii waweze kunufaika na tozo hii na itakayowasaidia kiuchumi.

Naye Bi. Doreen Anthony Sinare alieleza kuwa yeye na Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Hakimiliki Ndg. Victor Tesha wamepanga kufanya kikao na viongozi wa TAMRISO siku ya Alhamisi tar 19.10.2023 kupata taarifa ya mpango kazi wao na utekelezaji. Hivyo mara baada ya kikao hicho atawasilisha taarifa Wizarani.

Kuhusu maeneo ya kazi ambazo CMO hazijaomba, Bi. Doreen alieleza kuwa

“Tumetoa tangazo la kuongeza siku za wadau kuomba Leseni ya Kampuni ya Kukusanya Mirabaha kwa madaraja ambayo yalikuwa bado hayajaomba kama wadau wa Filamu, Sanaa za Ufundi na Wachapishaji wa Vitabu na mwisho wa kuwasilisha maombi hayo ni tarehe 02 Novemba, 2023. Baada ya kupokea maombi, Bodi ya COSOTA itapitia na kutoa maelekezo.”

Halikadhalika Naibu Waziri huyo ametoa wito kwa watu wote wanaofanya Uharamia na kazi za ubunifu kama Filamu, Vipindi, Muziki na Vitabu, sanaa za ufundi kuacha mara moja, pia ameiagiza COSOTA kufanya operesheni endelevu katika kupambana na uharamia, sababu hali hiyo inadidimiza kipato cha mmiliki wa kazi na kupoteza mapato yake halali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *