Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki, (Mb), akiongoza Mkutano Mkuu wa 25 wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) unaoendelea Jijini Samarkand, Uzbekistani leo Oktoba 18, 2023. Hatua hiyo imefuatia kuthibitishwa kwa Tanzania na Nchi Wanachama kuwa Makamu wa Rais wa Mkutano huo.
Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano Mkuu wa 25 wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki(Mb)(hayupo pichani) leo Oktoba 18, 2023.
WAZIRI KAIRUKI AONGOZA MKUTANO MKUU WA 25 WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki, (Mb), leo tarehe 18 Oktoba, 2023
ameongoza Mkutano Mkuu wa 25 wa UNWTO unaoendelea Jijini Samarkand, Uzbekistani. Hatua hiyo
imefuatia kuthibitishwa kwa Tanzania na Nchi Wanachama kuwa Makamu wa Rais wa Mkutano huo.
Akiongoza Mkutano Mkuu wa UNWTO Mhe. Kairuki amezishukuru nchi wanachama wa UNWTO kwa
kuichagua nchi ya Tanzania katika nafasi ya Makamu wa Rais na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na nchi
hizo ili kukuza na kuendeleza Sekta ya Utalii duniani.
Aidha, Waziri Kairuki alitoa pendekezo la kuanzishwa kwa Baraza au Jukwaa ambalo litajumuisha baadhi
ya waandishi wa habari, Watu Maarufu wenye ushawishi katika kijamii, waandishi wabobezi wa habari
za mtandao za utalii (travel bloggers)na wengine kwa lengo la kutangaza utalii duniani kote.
Mhe. Kairuki amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuiweka Sekta ya Utalii katika kiini cha maamuzi ya
kisiasa na kiuchumi kutokana na mchango wake kwenye ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na
maendeleo mengine.
“Tuungane sote kwa pamoja ili kuiinua zaidi sekta yetu ya utalii kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu
wetu” Mhe. Kairuki amefafanua.
Mkutano huo unaoendelea nchini Uzbekistani ulifungulia tarehe 16 Oktoba, 2023 na Rais wa Uzbekistan,
Mheshimiwa Shavkat Mirziyoyev na unahudhuriwa na Mawaziri wa Utalii kutoka Nchi wanachama wa
UNWTO zaidi ya 121 pamoja na Mashirika ya Kimataifa, Taasisi za kifedha na wadau kutoka sekta binafsi.