TAMASHA LA MICHEZO LA WANAWAKE LA TANZANITE 2023

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajimba tayari amewasili Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam kwa ajili ya Kufunga Tamasha la Michezo la Wanawake kwa mwaka 2023.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mussa Sima pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara hii Anastanzia Wambura pia wamehudhuria tukio hilo.

Tamasha hilo limeambatana na mada mbalimbali ikiwemo ya Uongozi na Utawala wa wanawake katika michezo iliyowasilishwa na Blandina Njau, Mtazamo wa jamii juu ya ushiriki wa wanawake katika michezo iliyowasilishwa na Bi. Irene Mwasaga na Mada ya Masoko, Matangazo na Udhamini iliyowasilishwa na Nandi Mwiyombella, mada zenye lengo la kuendelea kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *