WAZIRI NDUMBARO ATETA NA WAANDAJI WA SHEREHE ZA UFUNGUZI AFL

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Black Engineering kutoka nchini Italia Massimo Fogliati ambao ndio walioandaa sherehe za Ufunguzi wa African Football League Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamefanyika Oktoba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Waziri amewashukuru kwa kufanikisha ufunguzi huo, pamoja na kutoa ajira na fursa kwa watanzania ambao walihusika katika Ufunguzi huo.

Mhe. Ndumbaro amewakaribisha wawekezaji hao kufungua tawi hapa nchini kwakua tayari wana matawi Saud Arabia na Dubai.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji huyo, Bw. Massimo amepokea pongezi hizo na kushukuru Serikali na Wadau wote wa michezo kwa ushirikiano, ambapo ameahidi kurudi nchini kwa ajili ya kutafuta fursa zaidi na uwekezaji.

One thought on “WAZIRI NDUMBARO ATETA NA WAANDAJI WA SHEREHE ZA UFUNGUZI AFL

  1. Kitu kizuri lazima na ni muhimu kipongezwe ili wanaopongezwa waendelee kuwa na hamasa na kuongeza bidii zaidi.
    Nimesikitika tu kuwa mpaka sasa hatuna wazawa wenye uwezo wa kuandaa matukio makubwa hapa nchini kiasi cha kutafuta waandaaji kutoka nje. Hii ni biashara kubwa na fursa adhimu, ichangamkiwe na wazawa wapewe fursa za kuonesha uwezo wao.

    Fedha nyingi tunazokopa kwa ajili ya maendeleo zinarudi kwa wakopeshaji kwa njia kama hizo (kulipa kampuni na taasisi zao) huku tukiendelea kulipa deni lote na riba zake wakati kiasi cha fedha kinachobaki nchini kwa maendeleo ya kweli ni kidogo sana.

    Nadhani badala ya Waziri kuwaalika hao Black Engineering kuja kuwekeza hapa nchini, angetoa wito na rai kwa Watanzania kujifunza na kuwekeza kwenye maeneo hayo.
    Pia, angeomba fursa ya Watanzania kwenda kujifunza kwenye kampuni hiyo ili kama itatokea wakawekeza (Black Engineering)hapa nyumbani, wataalam wengi wa ngazi za juu wawe ni Watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *