WATUMISHI KANDA YA ZIWA WAASWA KUWA WABUNIFU KATIKA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO

Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi na Rasilimali watu Bw. William A. Kitebi pamoja na maafisa wengine, ilianza tarehe 18 Oktoba, 2023 na kutarajiwa kumalizika tarehe 25 Oktoba, 2023. Maafisa hao kutoka Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) walitembelea vituo vya Kanda ya Ziwa vikiwemo Makao Makuu ya Kanda ya Ziwa, Kituo Kidogo cha Mwanza, Mapori ya Maswa, Kijereshi na Ikorongo/Grumeti.

Wakiwa katika ofisi za Pori la Akiba Kijereshi jana tarehe 24 Oktoba, 2023 walipokelewa na Kaimu Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Ziwa ACC. Saidi I. Kabanda ambaye aliwakaribisha ili kuongea na Maafisa na Askari wa Kituo cha Makao Makuu ya Kanda ya Ziwa na Pori la Akiba Kijereshi.

Maafisa na Askari hao walipatiwa mafunzo yanayohusiana na mabadiliko ya muundo wa kiutumishi wa TAWA, jinsi ya kutumia mfumo wa Watumishi Portal (ESS), matumizi ya fomu zinazotolewa na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) pamoja na kuwasilisha maelekezo ya Kamishna wa Uhifadhi kwa Maafisa na Askari wote wa Mamlaka.

Katika Ziara hiyo, SAC – HR W.A. Kitebi aliwaasa watumishi wa Kanda ya Ziwa kufanyakazi kwa kuzingatia tunu za Mamlaka, kuwa wabunifu katika kufanyakazi na kuongeza ukusanyaji wa mapato.

Alisisitiza kuwa ‘Maafisa na Askari wawe na uwajibikaji katika utendaji kazi pamoja na kuendeleza utamaduni wetu wa umoja, uzalendo, uvumilivu, utii na ucha Mungu katika kudumisha uhifadhi na kuongeza ukusanyaji mapato.

Kamanda wa Uhifadhi wa Pori la Akiba Kijereshi C I E. Nkwama, alimshukuru Kamishna Kitebi kwa maneno ya faraja na maelekezo kwa maafisa na askari wa Mamlaka na kuahidi kwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka kuwa tutafanyakazi kwa bidii katika maeneo yote yanayosimamiwa na Mamlaka.

Aidha Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Ziwa ACC Saidi Kabanda alisema kuwa kwa sasa tumepata kiongozi mzuri, mlezi na anayejua kushughulika na hali zetu. Ameshukuru Kamishna Kitebi kwa maelekezo na maagizo aliyoyawasilisha na kusisitiza kuwa “ni Imani yetu kuwa watumishi tutabadilika na kuongeza ukusanyaji wa mapato

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *