WAKUU WA VITENGO VYA MAWASILIANO WAASWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza jambo wakati akifungua Kongamano la Wahariri wa vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi Maafisa Mawasiliano/ Masoko na Wahariri, kutumia kongamano hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa, kwa ustawi wa Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari, wa Kongamano hilo, Bw. Ben Mwang’onda, akimkaribisha Mgeni rasmi wa Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (hayupo pichani), kufungua kongamano hilo lililoandaliwa na Wizara hiyo ambalo linafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, mkoani Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akionesha chapisho la 19 la Ripoti ya Benki ya Dunia ya Hali ya Uchumi  ya Mwaka 2023, (Tanzania Economic Update-The Efficiency and Effectiveness of Fiscal Policy in Tanzania, wakati wa Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, lililoandaliwa na Wizara hiyo mkoani Morogoro, ambapo amewaelezea jinsi chapisho hilo linavyoonesha namna Tanzania inavyofanya vizuri katika maeneo mengi yaliyofanyiwa utafiti ikiwemo kuimarika kwa hali ya uchumi, mwenendo mzuri wa utoaji wa fedha kwenda kwenye miradi ya maendeleo, nchi kuwa na hifadhi ya fedha za kigeni za kutosha, kuimarika kwa ukusanyaji wa kodi za ndani, mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara pamoja na usimamizi mzuri wa Deni la Serikali na kushauri mambo kadhaa ikiwemo uimarishaji zaidi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kupitia kodi za ndani, usimamizi bora zaidi wa Bajeti Kuu ya Serikali na huduma nyingine za jamii.

Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, alipofungua Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kutumia kongamano hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa, kwa ustawi wa Taifa kwa ujumla.

Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma – PSPTB, Bi. Shamimu Mdee (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa (NIC) Karimu Meshack (wa pili kulia) na Meneja Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Amani Nkurlu (wa pili kushoto), wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine wamepata fursa ya kuelezea mafanikio na miradi mbalimbali ya taasisi zao kwa wahariri hao.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (katikati walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa vitengo vya Mawasiliano/ Masoko, kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, baada ya kufungua Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambalo limeandaliwa na Wizara ya hiyo, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kutumia Kongamano hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa, kwa ustawi wa Taifa kwa ujumla. Kulia walioketi ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja na  Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari wa Kongamano hilo Bw. Benny Mwang’onda.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (katikati walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari, baada ya kufungua Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha ambalo limeandaliwa na Wizara ya hiyo, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kutumia Kongamano hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa, kwa ustawi wa Taifa kwa ujumla. Kulia walioketi ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja na Kushoto ni Mwenyekiti wa Kongamano hilo la Wahariri, Bw. Ben Mwang’onda.

Na. Eva Valerian na Joseph Mahumi, WF, Morogoro
Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano vya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, wameaswa kuendelea kutangaza majukumu yanayofanywa na taasisi zao kikamilifu ili kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu miradi ama kazi zinazotekelezwa na Taasisi hizo na kuchangia kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati akifungua Kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano na Masoko vya Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari lililofanyika katika Ukumbi wa Nanenane, Mkoani Morogoro.
Aliwasisitiza Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wote kutumia jukwaa hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa kwa wadau, na kujadili changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi utakaoongeza ufanisi katika utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa maendeleo yao na ustawi wa Taifa kwa ujumla. 
Bi. Omolo alifafanua kuwa Mawasiliano ndio msingi wa mafanikio wa kila jambo, na kupitia mawasiliano Taarifa njema zinazohusu Taasisi zinaweza kusomwa na Wadau mbalimbali wa ndani na nje   na kuelewa mambo mazuri wanayoyatekeleza, hivyo wana wajibu wa kuhakikisha  kuwa wanazingatia Mawasiliano imara ya kimkakati ili kujenga Taswira chanya  kwa Wizara, Taasisi na Taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa lengo kuu la kongamano hilo lilikuwa kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa kwa wadau zinazohusu Wizara na Taasisi zake.
“Nimefarijika sana kuona kwamba mmeitikia wito wa kushiriki katika Kongamano hili, hii ni ishara njema kwa ustawi wa Wizara na Taasisi zake katika kukuza na kuimarisha Mawasiliano kwa Umma. Ni matumaini yangu kuwa siku za usoni kongamano hili litakuwa ni miongoni mwa makongamano bora na makubwa zaidi nchini” alisema Bi. Omolo.
Awali, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, aliwapongeza Wahariri na vyombo vya habari nchini kwa namna zinavyosukuma agenda ya Maendeleo na kutangaza habari zinazochagiza ukuaji wa uchumi wa nchi na kuifanya Tanzania iwe kinara katika Usimamizi na ukuaji wa uchumi katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.
Alisema kuwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, limesifu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kusimamia uchumi na Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa nchi inasimamia sera zake za uchumi na fedha kwa umahili
Naye Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari, wa Kongamano hilo, Bw. Ben Mwang’onda, aliishukuru Wizara ya Fedha kwa kuandaa kongamano hilo ambalo limekua daraja la mahusiano kati ya Wizara hiyo na Umma katika kutoa taarifa mbalimbali. 
Hilo ni Kongamano la pili la Mawasiliano kufanyika kati ya Wizara ya Fedha na Taasisi zilizo chini yake ambazo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Soko la Bidhaa Tanzania-TMX, Chuo cha Uhasibu Arusha-IAA, Mfuko wa Self-SELF Microfinance, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini – IRDP, Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma – PPAA, Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini – GPSA, Mfuko wa Uwekezaji – UTT-AMIS, Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi – PSPTB, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Ununuzi wa Umma – PPRA, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania – TIRA, Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika – EASTC, Benki ya Maendeleo ya Kilimo – TADB, Hazina Saccos na Shirika la Bima la Taifa – NIC.

Mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *