TANAPA YATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA KATIKA ULINZI WA MAENEO YA HIFADHI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na menejimenti ya TANAPA alipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za  Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa majukumu pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili ili kuzitatua,  leo jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na menejimenti ya TANAPA alipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za  Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa majukumu pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili ili kuzitatua,  leo jijini Arusha.

Baadhi ya Wakuu wa Vitengo na Idara wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za  Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) leo jijini Arusha.

Baadhi ya Wahifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za  Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) leo jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akikagua gwaride la heshima alipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za  Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa majukumu pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili ili kuzitatua,  leo jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akipokelewa na gwaride la heshima alipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za  Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) leo jijini Arusha.

TANAPA yatakiwa kutumia Teknolojia ya kisasa katika ulinzi wa maeneo ya Hifadhi

Na Happiness Shayo – Arusha

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetakiwa kutumia teknolojia ya kisasa kulinda na kuhifadhi maeneo yake kwa lengo la kuzuia ujangili na uvamizi wa maeneo hayo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.  Angellah Kairuki (Mb) ameyasema hayo leo Oktoba 28,2023 alipokuwa akizungumza na menejimenti ya TANAPA katika Ofisi za Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha.

” Kuhusu kukabiliana na ujangili pamoja na kufanya doria hifadhini tuendelee kuwa na matumizi ya vifaa vya teknolojia ya kisasa kuhakikisha doria na ulinzi wa maeneo yetu unafanikiwa kwa asilimia mia”amesema Mhe. Kairuki.

Amesema kwa kufanya hivyo, itawarahisishia utendaji kazi na kuwezesha ulinzi wa maeneo ya hifadhi kwa njia ya kisasa zaidi.

Aidha, ameitaka TANAPA kuendelea kutangaza vivutio vya utalii kidijitali  ili kufikia idadi ya watalii milioni tano kama ilivyokusudiwa.

“Muendelee kujiimarisha katika matumizi bora na sahihi ya kidijitali na pia mjikite katika kupata mrejesho wa huduma zinazotolewa kwa watalii  ili tuweze kuboresha huduma hizo” Mhe. Kairuki amesema.

Aidha, amewataka watumishi wa TANAPA kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria,  kanuni, taratibu  na miongozo iliyopo na kwa kutumia busara ili kulifanya shirika hilo lisonge mbele.

Mhe. Kairuki pia ameitaka menejimenti ya shirika hilo kushughulikia migogoro kati ya hifadhi na wananchi kwa kuhakikisha inapatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo na kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na wananchi kwa kuboresha ujirani mwema.

Naye, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Mussa Juma amesema atahakikisha anafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kuwa wabunifu kuhakikisha shirika hilo linasonga mbele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *