MHE. MWINJUMA AWAITA WAWEKEZAJI KUIBUA NA KUKUZA VIPAJI

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa rai kwa wadau mbalimbali wa michezo kuendelea kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kukuza michezo kwa kuwekeza ili kusaidia kuibua vipaji kuanzia kwenye vijiji na kata.

Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo Oktoba 28, 2023 baada ya kushuhudia mchezo wa fainali wa ligi ya Mbunge wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro, Mhe. Salim Alaudin Hasham na kugawa Kombe kwa mshindi ambapo pamoja na mambo mengine, alipata nafasi ya kuzungumza na wakazi wa kata ya Mwaya.

Fainali hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Shule ya Mwaya, imewakutanisha timu ya Gwasolly FC na Bodaboda Mawasiliano ambapo timu ya Gwasolly FC wameibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati baada ya mchezo kutamatika dakika 90 bila kufungana.

Bingwa wa ligi hiyo amepata zawadi ya TSH Milioni 26 ambapo Milioni 25 watachagua mahali pa kujenga darasa na milioni moja watagawana wachezaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *