MAPEMA LEO RAIS DKT SAMIA AMEFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA UJERUMANI MHESHIMIWA FRANK-WALTER STEINMEIER, AMBAYE YUKO NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU.

Rais Dkt Samia amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier, ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku tatu.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi yetu na Ujerumani umedumu kwa zaidi ya miaka sitini, na ni jukumu letu kuuendeleza na kuuongezea tija zaidi kwa manufaa ya mataifa haya mawili.

Ujerumani ni mbia wetu muhimu katika biashara na sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo maji, afya na mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *