TAMASHA LA KABILA LA WAMATENGO KUFANYIKA KILA MWAKA

Na Shamimu Nyaki

Tamasha la Utamaduni wa kabila la Wamatengo Mkoani Ruvuma litafanyika kila mwaka ili kutangaza utamaduni wa kabila hilo na Mkoa wa Ruvuma ndani na nje ya Tanzania.

Hayo yameelezwa Oktoba 30, 2023 na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati akifungua tamasha hilo katika kijiji cha Makumbusho Mtama Wilayani Mbinga.

“Matamasha haya yanatangaza Utamaduni, Mila na Desturi zetu watanzania, tamasha hili lifanyike kila mwaka ili kukumbushana maisha yetu ya asili, na nitoe rai kwa makabila mengine kuwa na Matamasha kama haya katika maeneo yao” amesema Mhe. Ndumbaro.

Tamasha hilo lilishereheshwa na burudani mbalimbali na kupambwa na maonesho ya tamaduni zenye asili ya kabila hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *