KATIBU MKUU WA WIZARA YA SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO, GERSON MSIGWA AMEKUTANA NA MABONDIA WALIOSHINDA MAPAMBANO YAO YA MIKANDA YA UBINGWA WA BARAZA LA NGUMI DUNIANI, WBC

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa mapema asubuhi ya Novemba Mosi amekutana mabondia walioshinda mapambano yao ya mikanda ya ubingwa wa Baraza la Ngumi Duniani, WBC na ubingwa wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini TPBRC katika ofisi za Baraza la Michezo BMT.

Mabondia hao ambao ni Fadhili Majiha aliyeshinda mkanda wa Ubingwa wa WBC Afrika alioshinda kwa kumshinda Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini wakati Pius Mpenda akishinda mkanda wa WBC Peace nchini Uturuki kwa kumchapa Dauren Yeleussino wa Kazakhstan huku Ibrahim Class akishinda ubingwa wa Taifa wa TPBRC dhidi ya Xiao Tau Su wa China.

Msigwa amewataka mabondia hao kuhakikisha wanaweza kujitunza ili waendelee kufanya vizuri katika mapambano yao wanayocheza kimataifa huku akitoa ahadi ya serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwaunga mkono kwenye mchezo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *