MSIGWA AITAKA COSOTA KUONGEZA MAPATO NA KUANDAA MIRADI

Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Hakimiliki Tanzania
(COSOTA) kwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg. Gerson
Msigwa alipotembelea Ofisi hiyo Oktoba 31, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg. Gerson Msigwa
(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ofisi ya Hakimiliki
Tanzania (COSOTA) mara baada ziara yake katika Ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Oktoba 31, 2023, wapili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki
Doreen Anthony Sinare na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Sanaa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

MSIGWA AITAKA COSOTA KUONGEZA MAPATO NA KUANDAA MIRADI
Na Anitha Jonas – COSOTA
Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg.Gerson Msigwa atoa
maelekezo kwa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuongeza vyanzo mapato
pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali itakayosaidia kuboresha utekelezaji wa
majukumu.
Mheshimiwa Msigwa ametoa maelekezo hayo Oktoba 31, 2023 katika kikao chake
na Menejimenti ya COSOTA alipotembelea Ofisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
“Katika kipindi cha uongozi wangu ninahitaji sana kuona Wizara na Taasisi
zinaonekana na zinasema utekelezaji wa shughuli zake, na kwa upande wa
COSOTA mnahitaji kujitangaza zaidi na kutoa elimu masuala haya ya hakimiliki
bado jamii haijui vizuri mnakazi kubwa katika kutekeleza hili” alisema Msigwa.
Akiendelea kuzungumza Katibu Mkuu huyo alishauri COSOTA kutazama Sheria
kama inaruhusu ili kuweza kufikiria suala la kupambana na uharamia utekelezaji
wake ufanywe Kampuni binafsi kwa usimamizi wa COSOTA ili kuweza kutekeleza
kwa ufanisi jukumu hilo kwa Tanzania nzima na kudhibiti watu wanaofanya shughuli
hizo.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Bi. Doreen Anthony Sinare
alimshukuru Katibu Mkuu huyo na kupokea maelekezo na ushauri ambapo aliahidi
kuyafanyia kazi na kutoa mrejesho.

Halikadhalika Doreen alieleza kuhusu Tozo ya Hakimiliki kuwa makusanyo
yameanza tar 1.9.2023 kwa ushirikiano na TRA ambayo vifaa vilivyoingizwa bado ni
vichache na aliomba nyongeza ya vifaa vingine ambavyo vinaendana na wakati
wasasa kuongezwa ili kusaidia ongezeko la makusanyo na kuboresha mapato ya
serikali, wasanii, waandishi na wabunifu mbalimbali katika masuala ya
hakimiliki.izara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

MWISHO***

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *