Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Dkt. Frank Walter Steinmeier akiweka Shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa vita ya Majimaji alipofanya ziara katika eneo hilo Novemba 1, 2023 Songea Mkoani Ruvuma.
Rais Mhe. Steinmeier ameambatana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali Laban Thomas na viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Dkt. Frank Walter Steinmeier akiweka ua katika kaburi la Chifu msaidizi (Nduna) Songea Luwafu Mbano, aliyezikwa katika eneo la Kumbukumbu ya Mashujaa wa Majimaji, alipotembelea eneo hilo Novemba 1, 2023 Songea Ruvuma.