Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa miradi yote inayopatiwa fedha na Serikali iliyopo Wizara ya Nishati itakamilika kwa wakati ili Sekta hiyo iwe na mchango mkubwa katika Pato la Taifa.
“Sisi wizarani tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha miradi yote ambayo fedha imetolewa na Serikali inakamilika kwa wakati,” amesema Dkt. Biteko.
Vile vile, amesema Wizara itashirikiana kwa karibu na kamati hizo ili kila jambo linaloshauriwa, kuelekezwa, linasimamiwa ipasavyo kwa manufaa ya umma hususan katika Sekta ya Nishati na Watanzania wote.