
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ufunguzi wa Chuo kikuu cha Teknolojia cha India nchini ni utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua rasmi chuo hicho Bweleo Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 06 Novemba, 2023.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa uwepo wa chuo hicho kwa Tawi la Zanzibar ni fursa adhimu kwa wataalamu wa ndani kubadilishana uzoefu na wataalam wa India hususani kwenye teknolojia ,utafiti na uvumbuzi.

Vilevile lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukifungua chuo hicho Zanzibar ni kuleta mabadiliko na mageuzi makubwa ya maendeleo ya nchi na watu wake kielimu, kiuchumi na kijamii.



