Waziri wa Ujenzi, innocent bashungwa ameziagiza Bodi za Usajili wa Makandarasi (CRB) na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), kuhakikisha zinaandaa mpango kazi wa kusimamia na kuimarisha taaluma ya Sekta ya Ujenzi nchini
ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wake ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia. Bashungwa ameyasemaa hayo leo Tarehe 06 Novemba, 2023 jijini Dodoma, alipokuwa akizindua Bodi za ushauri za CRB na ERB ambazo zinaundwa kwa mujibu wa sheria ili kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Bodi hizo.