Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amewataka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuongeza bidii ya ukusanyaji wa madeni kwa wapangaji wao na kuweka mikakati itakayowawezesha kukusanya madeni hayo ili kupata fedha za kujenga nyumba nyingine za kisasa na kuwezesha
watumishi wengi wa umma kupata huduma ya nyumba na makazi bora. Hatua hiyo inafuatia kutoridhishwa na kasi ya ukusanyaji madeni iliyopo sasa katika majengo yake nchini kote.