Na John Mapepele
Filamu ya The Royal Tour iliyochezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imezaa Epic Tanzania Tour.
Ziara hii ya awali ya EPIC ina wawekezaji 180 kutoka Marekani wanaotembelea Serengeti na Ngorongoro ambapo ziara pili itafanyika mwanzoni mwa Desemba na itajumuisha magwiji wa tennis duniani ambao watatoana jasho katikati ya Hifadhi ya Serengeti.
Miongoni mwa watopezi wa mchezo wa Tennis wanaotarajiwa kuwasili nchini ni Gigi Fernandez, John McEnroe pamoja na Mac Roy.
Program ya EPIC Tanzania Tour inaratibiwa na Kampuni ya Goshen Safari kwa kushirikiana na Serikali ambapo kundi hili linatarajiwa kuagwa rasmi na Serikali baada ya kuhitimisha ziara yake Novemba 12, 2023 ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe, Angellah Kairuki atatoa kauli ya Serikali.