Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), wameshiriki Mkutano wa Viongozi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), wameshiriki Mkutano wa Viongozi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika unaojadili namna ya upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira (Wash Leadership Summit), ulioandaliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha ya Ethiopia.
Mkutano huo unafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14 hadi 15 Novemba 2023, Jijini Addis Ababa, nchini Ethiopia.