Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) (katikati) , akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa (kulia), kabla ya kuanza kwa Mkutano wa viongozi wa Mashariki na Kusini mwa Afrika unaojadili namna upatikanaji wa maji safi, salama na usafi wa mazingira. Hii ikiwa ni hatua muhimu kwa nchi za Afrika kufikia malengo ya Maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals) ifikapo mwaka 2030.Kushoto ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb).