Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefungua Mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na masuala ya Fedha na Jinsia kutoka nchi 22 wanachama wa Jukwaa la Usawa wa Kijinsia (UN Women) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-Afritac East), katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo unalenga kujadili kuhusu namna ya kuwawezesha wanawake na wasichana kiuchumi na kijamii kupitia ufadhili wa usawa wa kijinsia. Pia, Viongozi hao watajadili namna bora ya kushughulikia athari za mapungufu ya kijinsia katika uchumi-jumla na kuchochea ufadhili wa masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kupitia bajeti za nchi zao ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Mawaziri wanaohudhuria Mkutano huo ni kutoka Tanzania, Burundi, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Eritrea, Ethiopia, Guinea, Ivory Coast, Nigeria, Senegal, Kenya, Liberia, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini, Rwanda, Sudan ya Kusini, Zambia, Zimbabwe na
Waziri wa fenda Mhe dkt mwigulu Nchemba akizungumza wakat wa mkutano wa mawaziri wa Afrika