RAIS, DKT. SAMIA KATIKA MAZUNGUMZO NA BAADHI YA MARAIS WA JUMUIYA AFRIKA MASHARIKI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kenya Mhe. Dkt. William Ruto, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Ndani Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ngurdoto Mkoani Arusha, tarehe 24 Novemba, 2023.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye kabla ya Mkutano wa ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ngurdoto Arusha 24 Nov, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Somalia, Mhe. Hassan Sheikh Mohamud, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ngurdoto Mkoani Arusha, tarehe 24 Novemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir Mayardit, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 24 Novemba, 2023.

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, akishiriki Mkutano wa Ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ngurdoto Mkoani Arusha, tarehe 24 Novemba, 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *