Washiriki wa Tamasha la World Happy Deaf Family Festival 2023 wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro Novemba 27, 2023 kujionea vivutio adhimu vya Wanyamapori.
Wakiwa katika hifadhi hiyo washiriki hao wameshuhudia makundi ya Wanyamapori wakiwemo simba, twiga, tembo, Nyati, nyumbu na swala chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Aidha, washiriki hao wamefanya utalii wa kuona Wanyamapori na kupiga picha ambayo ni fursa ya kuitangaza Tanzania katika nchi zao.
Tamasha hilo limehusisha washiriki zaidi ya 160 kutoka mataifa ya Afrika Kusini, Australia, Belarus, Brazil, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Guyana, Haiti, Hispania, India, Iran, Italia, Kenya, Kongo DRC, Malasia, Macedonia, Marekani, Mexico, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Pakistan, Poland, Romania, Rwanda, Senegal, Siera Leone, Sudan Kusini, Thailand, Tunisia, Jamhuri ya Czechoslovakia, Ufaransa, Uganda, Ujerumani, Ukraine, Urusi, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.