MBIO ZA KUDUMISHA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA INDIA KUFANYIKA DESEMBA 30

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili kuhusu tukio la mbio za pamoja za kudumisha ushirikiano kati ya Tanzania na India “The Friendship Run between India and Tanzania with Milind Soman” linalotarajia kufanyika jijini Dar es salaam kati ya tarehe 30 na 31 Desemba,2023.

Akizungumza kuhusu tukio hilo leo Desemba 5, 2023 Mhe. Ndumbaro amesema Serikali ya India imeomba ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kufanikisha tukio hilo ambalo litahudhuriwa na mwanariadha maarufu kutoka nchini India Milind Soman.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi.Neema Msitha, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt.Kiagho Kilonzo na Makamu wa rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, William Kallaghe.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *