WAZIRI MAKAMBA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA WIZARA MTUMBA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara unaoendelea katika mjini wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Lengo la kutembelea mradi huo ni kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi na kufanya mazungumzo na wasimamizi wa mradi ili kuwa baini uwepo wa changamoto zinazoweza kukwamisha ukamilishwaji wa mradi kwa wakati na viwango vinavyotarajiwa
Akizungumza na mkandarasi wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi Mhe. Makamba amepongeza hatua iliyofikiwa na amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo kuongeza kasi ili maradi huo ukamilike na kukabidhiwa kwa wakati.

“Pamoja na kazi nzuri iliyofanyika katika ujenzi wa jengo hili, bado kazi iliyobaki ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi ili mradi ukabidhiwe na jengo lianze kutumika na hatimaye kuleta haueni ya tatizo la uhaba wa ofisi kwa watumishi wa Wizara” amesema Mhe. Makamba


Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Makamba aliambatana na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samuel Shelukindo, na Balozi Stephen Mbundi anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki na watendaji wengine wa Wizara.

Jengo hilo litakalogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 22.9 hadi kukamilika kwake lilianza kujengwa mwezi Januari 2022. Ujenzi huo unaogharamiwa na Serikali unalenga kuziwezesha Wizara na Taasisi za Serikali kuwa na majengo ya kudumu katika mji wa Serikali.


Mradi wa ujenzi wa jengo hilo unatekezwa na Umoja wa makampuni ya Sole works na mshauri elekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *