Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametoa rai kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuweka sharti la lazima la kusoma somo la Kiswahili kwa wanafunzi ambao ni raia wa kigeni wanaojiunga na Chuo hicho.
Mhe. Ndumbaro amesema hayo leo Desemba 14, 2023 Mkoani Ruvuma wakati wa Mahafali ya 42 ya chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Majimaji mjini Songea.
Kiswahili ni bidhaa iliyo na wanunuzi wengi hivi sasa hivyo natoa rai kwenu uongozi wa Chuo kuweka sharti la lazima la kusoma somo la Kiswahili kwa wanafunzi raia wa kigeni wanaojiunga na Chuo”
Aidha Mhe. Ndumbaro ametoa rai kwa chuo hicho kianzishe kozi za muda mfupi na mrefu katika upande wa burudani na michezo.