MJI MPYA WA KISASA KUJENGWA ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekabidhiwa mfano wa ramani ya mji mpya wa biashara na uwekezaji, Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi .

Rais Dk.Mwinyi akipokea ramani hiyo Ikulu, Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe.Omar Said Shaaban , amepongeza hatua za awali zilizofikiwa na wazo la ujenzi wa mji huo.

Naye Waziri Shaaban alisema ujenzi wa mji huo wa kisasa utajumuisha ikiwemo ukumbi mkubwa wa mikutano wa kisasa wa kimataifa, hoteli kubwa za kisasa zenye hadhi ya nyota tano, ujenzi wa eneo la kisasa la biashara litakalohusisha maduka makubwa, Makaazi ya kisasa ya wananchi, ujenzi wa hospitali ya kisasa pamoja na kuwekwa viwanja vya michezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *