WAZIRI KAIRUKI AITAKA NCT KUTOA MAFUNZO YENYE UBORA NA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa maelekezo mbalimbali ya kuboresha utendaji kazi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho jijini Dar es Salaam Desemba 14,2023

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah  Kairuki(Mb) akikagua moja ya vyumba vya hoteli vinavyomilikiwa na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) chini ya Kampuni tanzu ya Utalii na Ukarimu, alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho jijini Dar es Salaam Desemba 14, 2023.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah  Kairuki(Mb) akikagua sehemu ya mafunzo ya kunyooshea nguo alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)  jijini Dar es Salaam Desemba 14, 2023.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na menejimenti ya Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kuhusu namna ya kutoa mafunzo bora na kuboresha mashirikiano na vyuo mbalimbali vya utalii duniani, alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho  jijini Dar es Salaam Desemba 14,2023.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na menejimenti ya Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kuhusu namna ya kutoa mafunzo bora na kuboresha mashirikiano na vyuo mbalimbali vya utalii duniani, alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho  jijini Dar es Salaam Desemba 14,2023.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na menejimenti ya Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kuhusu namna ya kutoa mafunzo bora na kuboresha mashirikiano na vyuo mbalimbali vya utalii duniani, alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho  jijini Dar es Salaam Desemba 14,2023. Wengine ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) (kushoto kwake), Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii ,Dkt. Florian Mtey (kulia), Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Edward Kohi (kulia kwake) na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Utalii ambaye ni Afisa Utalii Mkuu Kanda ya Pwani, Goodluck Mdumi.

Baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya Chuo cha Taifa cha Utalii(NCT) wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) alipokuwa akizungumza nao katika kikao kilichofanyika chuoni hapo Desemba 14,2023 jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah  Kairuki akikagua namna wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NC) wanavyoandaa mapishi, alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa chuo hicho, Desemba 14,2023 jijini Dar es Salaam.

WAZIRI KAIRUKI AITAKA NCT KUTOA MAFUNZO YENYE UBORA NA VIWANGO VYA KIMATAIFA
Na Happiness Shayo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekielekeza Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)
kujikita katika kutoa mafunzo yenye weledi, ubora na viwango vya hali ya juu ili kuendana na hadhi ya
utoaji huduma kwa watalii kimataifa.
Ameyasema hayo Desemba 14,2023 alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo cha Taifa cha Utalii kwa lengo
la kukagua utekelezaji wa majukumu yake pamoja kuzipatia ufumbuzi changamoto walizonazo.
“Tumeendelea kuwasisitiza kuhusiana na dhamana ambayo wamepewa na Serikali katika kuandaa
wahitimu wenye weledi, ubora na viwango vya hali ya juu ili watakapoenda huko wakatoe huduma
kwenye Sekta ya Utalii pamoja na maeneo ya uratibu wa matukio inayoakisi taswira ya Taifa letu” Mhe.
Kairuki amesema.
Aidha, Mhe. Kairuki amesisitiza juu ya suala la kuwaandaa vyema wakufunzi wa chuo hicho katika
masuala ya kitaalamu ya ukarimu, utalii, TEHAMA, kujiamini pamoja na kuwa na uwezo wa kumudu
lugha zaidi ya moja ili wawe na ushindani katika soko la ajira kitaifa na kimataifa.
Katika hatua nyingine Mhe. Kairuki ameitaka menejimenti ya chuo hicho kutafuta fursa mbalimbali na
kushirikiana na vyuo vingine vya utalii vya nje ya nchi kama Kenya, Ufaransa, Marekani na Canada ili
kuendelea kujifunza kutoka kwao.
Kwa upande wa miradi ya maendeleo Mhe. Kairuki amesema kwa kuwa chuo hicho kina Kampasi
mbalimbali jijini Arusha, Mwanza na Dar es Salaam kiangalie namna ya kuweza kudahili wanafunzi wengi
zaidi na kukidhi idadi na kiu ya kupata wataalamu ambao waajiri wangependa kuwapata.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za Waziri Kairuki za kujifunza namna Taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Maliasili na Utalii zinavyofanya kazi na kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *