Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema ushirikiano katika Sekta ya Utalii na Uhifadhi kati ya nchi ya Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China utazifaidisha nchi hizo kwa kukuza utalii pamoja na kuimarisha uhifadhi.
Ameyasema hayo usiku wa Desemba 15,2023 katika hafla fupi ya kulitangaza Jiji la Hangzhou la nchini China iliyofanyika kwenye ukumbi wa Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
”Nimefurahi kuona ushirikiano kati ya jiji la Hangzhou na Dar es Salaam unaanza hivyo tunatarajia kwamba ushirikiano huu utupe matokeo chanya zaidi na nchi zote mbili ziweze kufaidika hasa katika kukuza utalii wa jiji la Dar es Salaam” Mhe. Kairuki amesema.
Ameongeza kuwa kwa jinsi China ilivyo na utajiri mkubwa wa vivutio vya utalii pamoja na utangazaji utalii katika maeneo ya urithi na uhifadhi Tanzania itafaidika, lakini pia jiji la Dar es Salaam litafaidika.
Amewataka washiriki wa hafla hiyo kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania na kuwa mabalozi wa Utalii na uwekezaji kwa kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.
Na Happiness Shayo

Ametaja maeneo mbalimbali ya uwekezaji wanayoweza kuwekeza ikiwa ni pamoja na miradi mbalimbali ya mazao ya misitu kama mbao, shughuli za uwindaji, uhifadhi, huduma za malazi , huduma za usafiri na mnyororo mzima wa thamani wa mazao ya utalii.
Mhe. Kairuki ametumia fursa hiyo kuwasilisha ombi la kufungua soko la China katika uuzaji wa asali kutoka Tanzania kwa kuwa ni bidhaa yenye ubora.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya jiji la Hangzhou la nchini China, Bw. Li Huolin amesema jiji la Hangzhou linataka kupanua wigo wake wa ushirikiano na nchi nyingine duniani katika masuala ya kiuchumi na kibiashara.
“ Ni furaha yangu kubwa kuungana nanyi katika jiji hili zuri la Dar es Salaam kutafuta ushirikiano na maendeleo ya pamoja lakini pamoja na hilo, jiji la Hangzhou na Tanzania zina ushirikiano mkubwa na thabiti katika masuala ya kiuchumi na kibiashara” amesema Huolin.
Aidha, amesema ushirikiano baina ya China na Tanzania ni utekelezaji wa maafikiano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na ushirikiano wa kimkakati na kuendeleza urafiki wa kiutamaduni, kutengeneza fursa mbalimbali za kitaifa na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili” ameongeza Bw. Huolin.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka jiji la Hangzhou la nchini China kwenye sekta ya utamaduni na urithi, baadhi ya watendaji kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka sekta za utalii, makumbusho ya Taifa, utamaduni na urithi na sekta ya uwekezaji.