RAIS DKT. SAMIAH SULUHU HASSAN TUMEANZA JUMA LA MWISHO KUUFUNGA MWAKA 2023 LENYE SIKUKUU MBILI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Tumeanza juma la mwisho kuufunga mwaka 2023 lenye sikukuu mbili za Krismasi na Mwaka Mpya. Namuomba Mwenyezi Mungu ili sote tuweze kufikia siku hizi tukiwa wazima wa afya, kusherehekea kwa pamoja, kwa upendo, amani, furaha na usalama.

Katika sherehe hizi, baadhi yenu mnasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kujiunga na familia, ndugu, jamaa na marafiki. Nawasihi kuzingatia sheria ya usalama barabarani na kuchukua tahadhari na umakini mkubwa ili juma hili likawe lenye furaha, mkawe na muda mzuri na ndugu, jamaa na marafiki, na baadaye nyote mrejee mkiwa wazima wa afya kuendelea kufanya kazi ya kuliletea taifa letu maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *