WIZARA YA FEDHA, MIPANGO NA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA, MIFUGO, KUJA NA MPANGO KAZI ULIPO CHINI YA WIZARA HIZO

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), pamoja na Mawaziri wenzake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Profesa. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb), na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wamefanya kikao kazi cha pamoja kilichoshirikisha baadhi ya Taasisi zilizoko chini ya Wizara hizo.

Kikao kazi hicho kimejadili mambo mbalimbali ya kiutendaji yanayohusu Wizara hizo na Taasisi zake. Aidha, Kikao hicho kimewahusisha Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Gilead Teri pamoja na wataalam wengine kutoka katika Wizara na Taasisi hizo.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Hazina Ndogo Jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *