DKT. NCHEMBA ATETA NA WAZIRI WA VIWANDA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta ya viwanda na Biashara ili sekta hiyo iweze kuongeza mchango wake katika Uchumi na maendeleo ya watu. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akieleza utekelezaji wa miradi wakati alipoongoza ujumbe wa Wizara yake walipokutana na ujumbe wa Wizara ya Fedha ukiongozwa na Waziri wake Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwa ajili ya kujadili maendeleo ya sekta ya viwanda na biashara nchini. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sheria Wizara ya Fedha, Bi. Mwantumu Sultan, akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), walipokutana na kujadili maendeleo ya sekta ya Viwanda na biashara. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma.  Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Idara Uchambuzi wa Sera wa Wizara ya Fedha, Bw. Mbayani Saruni.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Viwanda na Biashara,  akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule, akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha ukifuatilia mkutano kati ya Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hawapo pichani), ulioangazia maendeleo ya Wizara ya Viwanda na Biashara, uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma. 

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto), wakiwa katika kikao kilichowashirikisha wajumbe kutoka pande hizo mbili kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma. 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano  ya Serikali, Wizara ya Fedha)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *