MHE: NDUMBARO AMKARIBISHA WAZIRI WA MICHEZO IVORY COAST KWENYE DERBY YA KARIAKOO KUMUONA PACOME

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast Mhe. Adjé Silas ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili kuhusu ushirikiano wa nchi hizo kwenye Sekta ya michezo ambapo Mhe. Ndumbaro amemualika Mhe.Silas kushuhudia mechi ya Derby ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Aprili 20, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ili aone ladha ya mechi hiyo kubwa Afrika Mashariki pamoja na kuwaona wachezaji nyota wa timu hizo akiwemo mchezaji Pacome Zouzoua wa Yanga ambaye ni raia wa Ivory Coast.

Mhe. Silas yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pia atashiriki hafla ya kuingia makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ivory Coast katika sekta ya michezo itakayofanyika Aprili 21, 2024 Jijini Dar Es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *