Kamishna mpya wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Dkt. Elirehema Doriye aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameripoti katika makao makuu ya Ofisi hiyo kwa ajili ya kuanza Majukumu yake mapya.
Dkt. Doriye amepokelewa na Menejimenti ya NCAA na baadae kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Kamishna wa Uhifadhi NCAA Richard Kiiza.