WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO ZA MBEYA TULIA MARATHON 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 11, 2024 ameshiriki katika tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathoni 2024 zilizoandaliwa na Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Tulia Trust. Mbio hizo zilianzia na kuishia kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Mei 11, 2024.

Baadhi ya viongozi walioshiriki mbio hizo ni Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma, Wakuu wa Mikoa ya Njombe na Mbeya, Wabunge na Viongozi wa Vyama vya Siasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *