BALOZI WA TANZANIA NCHINI MSUMBIJI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA BODI YA UTALII TANZANIA WATETA FURSA ZA UTALII

Mhe. Balozi Phaustine Kasike akutana na Bw. Ephraim Balozi Mafuru, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii (TTB).

Katika Mkutano huo, Bw. Mafuru alimueleza Balozi Kasike kwamba katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, TTB imeamua kufanya kazi kwa ukaribu na Taasisi mbalimbali ikiwemo Balozi za Tanzania nje ya nchi ili kuongeza idadi ya watalii kutoka nje. Hivyo, alimuomba Balozi Kasike kuipatia Ofisi yake malengo na mikakati ya Ubalozi katika kuiwezesha Tanzania kunufaika na Sekta ya Utalii ili kuweka mikakati ya pamoja kwa maslahi ya nchi.

Mhe. Balozi aliahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa TTB ili Taasisi hiyo iweze kufikia malengo yake. Aidha, aliahidi kuiunganisha Taasisi hiyo na Taasisi zinazohusika na Sekta ya Utalii ili kuangalia uwezekano wa kuwa na mashirikiano.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania – Maputo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *