Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), yuko Madrid, Hispania ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara, na Utalii wan chi hiyo, Bi. Xiana Mendez, ambapo Hispania imeihakikishia Tanzania kuwa iko tayari kuendelea kushiriki katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kupitia Taasisi yake (Export Credit Agency-ECA), kwa kutoa mikopo, dhamana ya mikopo na Bima kwa kampuni za nchi hiyo zitakazojenga reli hiyo kuanzia Makutopora hadi Mwanza na Kipande cha kuanzia Tabora – Kigoma hadi Malagarasi, kutokana na umuhimu wa mradi huo kwa maendeleo ya nchi.