Na Shamimu Nyaki
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameongoza ujumbe wa Tanzania kutembelea Ubalozi Cairo nchini Misri kabla ya siku ya kupiga kura ya kupata nchi mwenyeji wa Mashindano ya Afrika (AFCON 2027) itakayopigwa Septemba 27, 2023 nchini humo.
Dkt. Ndumbaro amesema Tanzania, Kenya na Uganda kupitia Marais wa nchi hizo wako tayari kwa ajili ya mashindano hayo kwa kuwa zina mazingira mazuri ikiwemo miundombinu ya michezo ambayo ipo na inakidhi mashindano hayo, usafiri na malazi ya kutosha katika nchi hizo unaochagizwa na maeneo mazuri ya Utalii.
Naye Mhe. Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema atahakikisha anawashawishi Mabalozi wa nchi mbalimbali kuunga mkono fursa hiyo adhimu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia amesema nchi hizo zinayo nafasi ya kushinda kwakua hazijawahi kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ambapo amesema viwanja tisa vitatumika katika nchi hizo.